Psalms 112:2-9


2 aWatoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi,
kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa.
3 bNyumbani mwake kuna mali na utajiri,
haki yake hudumu milele.
4 cHata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu,
yule mwenye rehema, huruma na haki.

5 dMema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba,
anayefanya mambo yake kwa haki.
6 eHakika hatatikisika kamwe,
mtu mwenye haki atakumbukwa milele.
7 fHataogopa habari mbaya,
moyo wake ni thabiti, ukimtegemea Bwana.
8 gMoyo wake ni salama, hatakuwa na hofu,
mwishoni ataona ushindi dhidi ya adui zake.
9 hAmetawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini;
haki yake hudumu milele;
pembe yake itatukuzwa kwa heshima.
Copyright information for SwhNEN